WENYEJI, Paris Saint-Germain wamepata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa kwanza Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumanne Uwanja wa Parc des Princes Jijini Paris, Ufaransa.
Bao pekee la PSG limefungwa na Kylian Mbappe dakika ya 90 na ushei katika mchezo ambao Muargentina Lionel Messi alikosa penalti baada ya mkwaju wake kuokolewa na kipa Thibaut Courtois.
Penalti hiyo ilitolewa baada ya beki Dani Carvajal kumchezea rafu Mbappe kwenye boksi dakika ya 62.
Penalti hiyo ilitolewa baada ya beki Dani Carvajal kumchezea rafu Mbappe kwenye boksi dakika ya 62.
0 comments:
Post a Comment