ALIYEWAHI kuwa Katibu Mkuu klabu ya Yanga miaka ya 1980, Issa Makongoro amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa taarifa ya familia yake zinasema msiba uko Mikocheni kwa Warioba na maziko yatafanyika leo Makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.
Uongozi wa Yanga SC umesema umepokea kwa msikitiko makubwa taarifa ya msiba wa kiongozi wake huyo wa zamani, enzi za mfumo wa Makatibu wa kuchaguliwa kwa kura za wachama, tofauti na sasa watendaji wa nafasi hizo wanaajiriwa.
0 comments:
Post a Comment