WENYEJI, Manchester City wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Brentford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatano Uwanja wa Etihad.
Mabao ya Man City yamefungwa na Mualgeria Riyad Mahrez dakika ya 40 kwa penalti baada ya Raheem Sterling kuchezewa rafu na Mads Roerslev wa Brentford na la pili, Mbelgiji Kevin de Bruyne dakika ya 69 akinufaika na makosa ya David Raya.
Sasa kikosi cha kocha Mspaniola, Pep Guardiola, Manchester City kinafikisha pointi 60 katika mchezo wa 24 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 12 zaidi ya Liverpool inayofuatia ambayo pia ina mechi mbili mkononi, wakati Brentford inabaki na pointi zake 23 za mechi 24 sasa katika nafasi ya 14.
0 comments:
Post a Comment