WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi wa 6-0 dhidi ya Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield usiku wa Jumatano.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Mohammed Salah kwa penalti yote mawili, dakika ya 15 na 35, Joel Matip dakika ya 30, Sadio Mane mawili pia dakika ya 80 na 90 na beki Virgil Van Dijk dakika ya 90 na ushei.
Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 60, sasa ikizidiwa tatu tu na Mabingwa watetezi, Manchester City baada ya timu zote kucheza mechi 26, wakati Leeds inabaki na pointi zake 23 za mechi 25 nafasi ya 15.
0 comments:
Post a Comment