WENYEJI, Geita Gold wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
Mabao ya Geita Gold yamefungwa na George Mpole kwa penalti dakika ya 38 na Danny Lyanga dakika ya 41 na kwa ushindi huo, Geita Gold inafikisha pointi 20 katika mchezo wa 15 na kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi katika nafasi ya nne.
Coastal Union, mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 1988, wanakamilisha mechi 15 za mzunguko wa kwanza wa Ligi wakiwa na pointi 17 katika nafasi ya tisa.
Mechi nyingine wa Ligi Kuu leo, wenyeji, Polisi Tanzania wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Kagera Sugar Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kagera Sugar inafikisha pointi 20 na kushuka kwa nafasi moja hadi ya saba, wakati Polisi inafikisha pointi 19 katika nafasi ya nane baada ya timu zote kukamilisha mechi 15 za mzunguko wa kwanza wa Ligi.
0 comments:
Post a Comment