TIMU za Coastal Union na Kagera Sugar zimefanikiwa kuingia Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi dhidi ya wageni, Mtibwa Sugar na Namungo jioni ya leo.
Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga mabao ya Coastal Union dhidi ya Mtibwa yamefungwa na Haji Ugando dakika ya 10 na Abdul Suleiman ‘Sopu’ dakika ya 90 na ushei na Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera bao pekee la Kagera limefungwa na Hassan Mwaterema dakika ya 60.
Coastal na Kagera zinaungana na Geita Gold iliyoitoa Mbuni FC na Azam FC ilitoitupa nje Baga Friends kutinga Robo Fainali ya michuano hiyo maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
0 comments:
Post a Comment