WAFANYAKAZI 12 Azam Media Limited (AML) wamepata ajali katika eneo la Mlima Kitonga, Iringa mchana wa leo wakiwa njiani kwenda mkoani Mbeya kwa ajili ya kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Gari lililowabeba wafanyakazi hao lilisukumwa na lori lililokuwa likirudi nyuma kwa dharura katika mlima huo mkali.
Mara baada ya ajali hiyo, majeruhi walichukuliwa na matabibu wa Mkoa wa Iringa kwa matibabu kwa msaada mkubwa wa ofisi ya mkuu wa Mkoa, kikosi cha Polisi Mkoa wa Iringa na Mganga mkuu wa Mkoa.
Uongozi wa Azam Media Limited umewashukuru wote waliotoa msaada wa hali na mali na kuwaomba Watanzania wote kuwaombea majeruhi nafuu ya mapema.
0 comments:
Post a Comment