WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na washambuliaji wake wa kigeni, Mzambia Rodge Kola dakika ya tano na Mkongo, Idris Mbombo dakika ya 64.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 14 na kupanda nafasi ya tatu, ikiizidi pointi mbili Mbeya City ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi.
Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 17 za mechi 14 sasa baada ya kucheza mechi 14 pia katika nafasi ya nane.
0 comments:
Post a Comment