WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Brentford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Emirates Jijini London.
Arsenal inafikisha pointi 42 katika mchezo wa 23, ingawa inabaki nafasi ya sita, wakati Brentford inabaki na pointi zake 24 za mechi 26 katika nafasi ya 14.
Mabao ya Arsenal yamefungwa na Emile Smith Rowe dakika ya 48 na Bukayo Saka dakika ya 79, wakati la Brentford limefungwa na Christian Norgaard dakika ya 90 na ushei.
0 comments:
Post a Comment