MWILI wa aliyewahi kuwa beki wa timu ya taifa ya Tanzania, Ally Abdulkarim Ibrahim Mtoni ‘Sonso’ (28) umezikwa jana jioni katika makaburi ya Ndugumbi, Magomeni Jijini Dar es Salaam.
Ally Sonso aliyezaliwa Machi 13, mwaka 1993 Jijini Dar es Salaam alifariki dunia Ijumaa wakati akikimbizwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam kwa matibabu kutokana na maumivu ya mguu yaliyoanza kumsumbua Oktoba mwaka jana.
Kisoka, Ally Sonso aliibukia timu ya vijana ya Villa Squad ya Magomeni, kabla ya kwenda Lipuli ya Iringa, baadaye Yanga, Kagera Sugar na Ruvu Shooting. Alikuwemo kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichoshiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 nchini Misri. RIP.
0 comments:
Post a Comment