MABINGWA wa Afrika, Al Ahly wametupwa nje ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Palmeiras ya Brazil katika mchezo wa Nusu Fainali usiku wa Jumanne Uwanja wa Abu Dhabi.
Alikuwa ni kiungo mwenye umri wa miaka 26, Raphael Veiga aliyefunga bao la kwanza dakika ya 39, kabla ya mshambuliaji Eduardo Pereira Rodrigues ‘Dudu’ kufunga la pili dakika ya 49.
Na sasa mabingwa hao wa Amerika Kusini, Palmeiras watakutana na mshindi kati ya bingwa wa Asia, Al-Hilal na bingwa wa Ulaya, Chelsea wanaomenyana leo usiku Uwanja wa Mohammed bin Zayed.
Al Ahly itawania nafasi ya tatu dhidi Al Hilal au Chelsea.
0 comments:
Post a Comment