KLABU ya Simba imeandikia barua Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) kuhoju juu ya mkataba wa udhamini wa kampuni ya GSM katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara huku pia wakiwa wadhamini wa wapinzani wao, Yanga SC.
Katika barua hiyo iliyosainiwa na Mtendaji Mkuu wa Simba, klabu hiyo imesema haifahamu kwa undani juu ya mkataba huo wao watanufaika vipi zaidi tu ya kufahamishwa kutumia nembo ya GSM kwenye tiketi na jezi zao wakati wa mechi za ligi hiyo.
Lakini pia Simba imesema GSM kuwa wadhamini wa Ligi Kuu wazi inaleta mgongano wa kimslahi kwa sababu ni wadhamini wa Yanga pia, klabu ambayo kwa pamoja na mdhamini wao lengo lao ni kutwaa ubingiwa ligi kama wao.
Novemba 23, mwaka huu GSM iliingia mkataba wa Udhamini Mwenza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa dau la Sh. Bilioni 2.1 kwa miaka miwili.
0 comments:
Post a Comment