MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamepangwa Kundi D katika Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na RS Berkane ya Morocco wanayochezea Mzambia, Clatous Chama na Mkongo, Tuisila Kisinda.
Chama aliwika Simba kwa misimu mitatu tangu 2018, kabla ya kuuzwa RS Berkane Julai mwaka huu, wakati Kisinda alicheza kwa watani wao, Yanga msimu mmoja kabla ya kuuzwa pia mwanzoni mwa msimu huu.
Timu nyingine katika Kundi D ni ASEC Mimosa ya Ivory Coast na US Gendarmerie ya Niger, wakati Kundi A kuna Pyramids ya Misri, CS Sfaxien ya Tunisia, Al Ahly Tripoli ya Libya na ZANACO ya Zambia.
Kundi B kuna TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), AS Otohi ya Kongo-Brazzaville, Cotton Sport ya Cameroon na Al Masry ya Misri na Kundi C zipo JS Soura ya Algeria anayaochezea mchezaji mwingine wa zamani wa Simba, Adam Salamba, Al Ittihad ya Libya, Orlando Pirates ya Afrika Kusini na mshindi wa jumla kati ya JS Kabylie ya Algeria na Royal Leopard ya Eswatini.
Royal Leopard iliilaza JS Kabylie 1-0 katika mechi ya kwanza nyumbanii, kabla ya mechi ya marudiano kusogezwa mbele hadi Januari kwa sababu ya COVID 19.
0 comments:
Post a Comment