KIUNGO Salum Abubakar 'Sure Boy' ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa kwanza wa Yanga SC katika dirisha dogo la usajili.
Sure Boy anajiunga na Yanga, timu ambayo baba yake aliichezea kati ya mwaka 1986 na 1993 baada ya kuachana na Azam FC aliyojiunga nayo mwaka 2007.
Sure Boy ameandika katika ukurasa wake wa Instagram kuishukuru Azam FC kwa kumkuza kisoka.
"Assalam Alaykum, Nitumie Fursa Hii Kushukuru Management, Technical Staff, Makocha, Viongozi, Mashabiki, Wachezaji Wenzangu Na Wafanyakazi Wote Wa @azamfcofficial Tuliofanya Kazi Kwa Pamoja Kwa Ushirikiano Kwa Kipindi Kirefu Sana.
Nyakati Za Huzuni, Majonzi Na Furaha Zote Tulisimama Pamoja Kuipigania Team Kwa Jasho Na Damu.
Nimeishi Kama MwanaFamilia Kwa Miaka Yote Hapo Klabuni, Nilikuja Nikiwa Kijana Mdogo Sana .
Naondoka Kutafuta Changamoto Mpya Nikiwa Nimepuvuka Kimwili Na Kiakili.
Mimi Ni Binaadamu Kama Kuna Sehemu Nimewakosea Naombeni Mnisamehe Na Mimi Pia Nimesamehe Kama Mlinikosea.
Asanteni Sana @azamfcofficial Nathamini Mchango Wenu Mkubwa Katika Maisha Na Career Yangu Kwa Ujumla," amemalizia Sure Boy.
Abubakar Salum 'Sure Boy' enzi zake anacheza Yanga, hapa anamtoka beki wa Simba SC, Iddi Selemani 'Meya' katika moja ya mechi za Ligi Daraja la Kwanza (sasa Ligi Kuu) Tanzania Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru), Dar es Salaam mwianzoni mwa miaka ya 1990. |
0 comments:
Post a Comment