MWANAHISA Mkuu wa klabu ya Simba, Mohamed 'Mo' Dewji ameahidi kutoa Sh. Bilioni 2 ili wanachama wajazie klabu hiyo ijenge Uwanja wake kwa mechi zake za mashindano ya ndani na ya Kimataifa.
"Nimepokea maoni mengi ya WanaSimba wenzangu wakishauri tujenge uwanja wetu na wako tayari kuchangia ili tufanikishe ujenzi huo," ameandika Dewji katika ukurasa wake.
"Naomba kuweka wazi kwamba nimepokea maoni hayo kwa mikono miwili. Naomba Bodi ya Simba kukaa na kuja na utaratibu wa haraka ili jambo hili lianze utekelezaji,".
"Kwa kuanza naahidi kuchangia Tsh. 2 bilioni. Nawaomba wanasimba tuchangie sote,".
Kwa sasa Simba ina Uwanja wa mazoezi tu, Mo Simba Arena uliopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na mechi zake za mashindano inatumia Uwanja wa Benjamin Mkapa.
0 comments:
Post a Comment