WENYEJI, Azam FC wamefanikiwa kwenda Raundi ya Nne Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Green Warriors usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na washambuliaji Mkongo, Idris Mbombo dakika ya nne, Prince Dube Mpumelelo mawili dakika ya 65 na 86 na Mzimbabwe mwenzake, kiungo Never Tigere dakika ya 85.Ulikuwa mchezo wa kwanza Azam FC baada ya kumfukuza kocha Mzambia, George Lwandamina, ukimpa mwanzo mzuri kocha anayekaimu, Mmarekani mzaliwa wa Somalia, Abdihamid Moalin.
0 comments:
Post a Comment