WENYEJI, Kagera Sugar wamechapwa mabao 2-0 na Mbeya Kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Mabao ya Mbeya Kwanza jioni ya leo yamefungwa na Willy Edgar dakika ya 36 na Oscar Mwajanga dakika ya 85 na kwa ushindi huo inafikisha pointi 10 katika mechi ya 10 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Kagera inabaki na pointi zake tisa za mechi tisa nafasi ya 11.
Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Namungo FC imekubali kipigo cha 2-1 kutoka kwa Dodoma Jiji FC Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
Mabao ya Dodoma Jiji yamefungwa na Anuary Jabir dakika ya 18 na Emmanuel Martin dakika ya 73, wakati la Namungo FC limefungwa na Bigirimana Blaise dakika ya 26.
Dodoma Jiji FC inafikisha pointi 16 katika nafasi ya nne, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake 12 katika nafasi ya saba baada ya timu zote kucheza mechi 10.
0 comments:
Post a Comment