LIGI Kuu ya Wanawake Tanzania Bara inatarajiwa kuanza keshokutwa kwa timu zote 12 kushuka dimbani.
Mabingwa watetezi, Simba Queens watafungua dimba na Ruvuma Queens Uwanja wa Mo Simba Arena, wakati washindi wa pili wa msimu uliopita, Yanga Princes wataanzia ugenini dhidi ya Baobao Queens Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma Desemba 24.
Watani wa jadi, Simba Queens na Yanga Princes wakikutana Januari 8, mwakani Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment