WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC la kwanza alijifunga Michael Masinda dakika ya 20, Ismail Aziz dakika ya 44, Charles Zullu dakika ya 50 na Tepsi Evance dakika ya 81, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na Saadat Mohamed dakika ya 63.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 15 na kusogea nafasi ya sita, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake tisa katika nafasi ya 13 baada ya timu zote kucheza mechi 10.
0 comments:
Post a Comment