KAMPUNI ya Star Media (T) Limited kupitia chapa yake ya Startimes imethibitisha kushirikiana na Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kuonyesha LIVE kombe la mataifa ya Africa 2021(AFCON 2021).
AFCON 21 itapigwa nchini Cameroon, Startimes imepata haki za matangazo kurusha michezo yote 52 ya michuano hii, yaani kuanzia tarehe 9 Januari 2022 mpaka Februari 6, 2022.Timu kuu shiriki ni pamoja na Senegal, Misri, Morocco, Tunisia, wenyeji Cameroon, Ivory Coast, Ghana na mabingwa watetezi Algeria.
StarTimes itarusha michezo hii kupitia chaneli za michezo za ST. World Football (Kiingereza), Sports Premium (Kifaransa) pamoja na TV3 kwa Lugha ya Kiswahili.
Ili kuweza kutazama michezo hii moja kwa moja lipia kifurushi chako cha Mwezi cha Dish (Smart) Tsh 21,000 na Antenna (Uhuru) Tsh 20,000.
0 comments:
Post a Comment