// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); GYNAH ASHINDA TUZO ZA LIPFF KENYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE GYNAH ASHINDA TUZO ZA LIPFF KENYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, November 08, 2021

    GYNAH ASHINDA TUZO ZA LIPFF KENYA


    MWANDISHI, muigizaji na mwanamitindo, Regina Kihwele 'Gynah', mwanamziki ameibuka mshindi wa  muigizaji bora kike kwenye tuzo  za Lake International Pan African Film Festival(LIPFF) zilizofanyika usiku wa tarehe 6 November mwaka 2021, nchini Kenya na kuwabwaga waigizaji wengine kutoka, Afrika Kusini ,Cameroon, Morocco na Uganda
    Tanzania  ilikuwa  pia kwenye kinyang'anyiro cha muigizaji bora kwa wanaume. Cojack Chilo aliyeigiza kwenye filamu ya "Nyara the kidnapping" aliteuliwa kushindana na nchi na Ghana, Uganda, Kenya, Afrika Kusini ambapo Rushabiro Raymond kutoka Uganda aliyeigiza filamu iitwayo "Stain" alishinda tuzo hiyo. 
    Pia kwenye kikundi cha filamu bora kipengele filamu ya "Nyara the kidnapping" kutoka Tanzania ilikuwa ikishindanishwa na wateuliwa watatu kutoka Kenya na Uganda na tuzo ilienda kwa filamu ya Mission to rescue kutoka Kenya.
    KUHUSU MULASI:
    Mulasi ni neno la “kigogo” ambalo kwa Kiswahili linamaanisha "Rafiki". Kabila la wagogo linapatikana mji mkuu au makao makuu ya Tanzania ambayo ni Dodoma. Mulasi (rafiki yangu) ni filamu kuhusu mwanamke aitwaye Sechelela ambaye an usongo wa mawazo ambapo anapitia kipindi kigumu kati yake na familia yake pia na kazi zake. Marafiki zake huwa pamoja naye wakati wote kumfariji wakiwa kwenye safari yao ya kutalii mji wa Dodoma.
    Filamu imeongozwa na Honeymoon Aljabri mwenye tuzo za utengenezaji na uongozaji filamu, aliyezaliwa na kukulia Dodoma, Tanzania lakini makao yake ni Marekani. Honeymoon aliona bora kuigiza filamu hii mkoa alipozaliwa, Dodoma ili kukuuza utalii wake ambao bado haujachunguzwa na kuelezea filamu hii kwa lugha ya Kiswahili ili kuweza kukuza lugha na utamaduni wa nchi yake, Tanzania. Ameogelea mada ya kuhusu afya ya akili ili kuweza kuungana na hadhira ya kitanzania na ya kimataifa ambapo mada hii watu hupuuzia mara nyingi.
    Regina Kihwele ni binti mwenye vipaji vingi aliyeigiza kama muigizaji mkuu Sechelela. Sechelela ni mwanamke jasiri anayebeba machungu mengi ambayo wanawake wengi wakitanzania kwenye ndoa zao huficha.
    Tuzo hizi zimekuwa daraja la kukuza sekta ya filamu na utalii ya Tanzania kupitia waigizaji wadogo wadogo wa kike walioshinda tuzo hizo. Regina kama msanii na mtetezi wa afya ya akili anaamini kuwa filamu hii ni njia rahisi ya kueneza uelewa kwenye jumuiya ya Tanzania. Yeye anajiona kama mhamasishaji kwa waigizaji wengine wakike wenye matamanio na pia kuwa kama sehemu ya harakati kutamsaidia yeye kufanikiwa kwenye ndoto zake za kutengeneza filamu za aina ya elimu - burudani kutoka Tanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GYNAH ASHINDA TUZO ZA LIPFF KENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top