BEKI wa timu ya taifa ya soka ya wasichana chini ya miaka 20 ya Tanzania, Tanzanite, Fumukazi Nguruwe amefungiwa mechi tatu za michuano ya CECAFA Challenge U20 inayoendea nchini Uganda.
Taarifa ya Baraza la Vyama vya soka Afrika Mashariki na kati (CECAFA) leo imesema mchezaji huyo amefungiwa baada ya kukutwa na hatia ya kumfanyia vurugu Mwamuzi wakati wa mchezo dhidi ya Ethiopia, ambao Tanzania ilifungwa 2-1.
Kamati ya Nidhamu ya CECAFA pia imemfungia mchezo mmoja Mtunza vifaa wa Tanzanite, Esther Chabruma kwa kumtolea lugha isiyofaa Mwamuzi wa mchezo huo.
Kamati hiyo pia imewaonya wachezaji wawili wa Tanzania, Emiliana Mdimu na Mwamvua Haruna kwa kujihusisha na vurugu hizo huku timu hiyi ikipigwa faini ya dola za kimarekani 500.
Tukio hilo lilitokea baada ya refa kukataa bao lililofungwa na Aisha Masaka ambalo lingekuwa la kusawazisha.
0 comments:
Post a Comment