SHIRIKISHO la SOKA Tanzania (TFF), limesema halihusiki na kufukuzwa kwa kocha yeyote wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kama inavyopotoshwa na baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii.
Taarifa ya TFF imesema kwamba klabu zote za Ligi Kuu zilikamilisha taratibu za kusajili maafisa wake wa benchi la Ufundi na walipitishwa wote kwa mujibu wa taratibu.
Taarifa ya TFF inafuatia madai kwamba Simba SC imewafukuza makocha wake wa kigeni kwa sababu walizuiwa na shirikisho hilo kufanya kazi nchini kwa sababu hawana sifa.
Simba ilitangaza kuachana na Kocha wake, Didier Gomes Da Rosa siku mbili baada ya timu kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia kuchapwa 3-1 nyumbani na Hwaneng Galaxy Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Pamoja na Gomes, wameondolewa pia kocha wa makipa, Mbrazil Milton Nienov na ko cha wa viungo, Mtunisia Adel Zrane – wanabaki Mnyarwanda Hitimana Thierry na Suleiman Matola.
0 comments:
Post a Comment