SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limekanusha kumuombea uraia mshambuliaji wa Simba SC, Kibu Dennis Prosper.
Taarifa ya TFF imesema si kweli kwamba rais wa shirikisho hilo, Wallace John Karia amesema alimuombea uraia Kibu kwa sababu anahitajika kwa ajili ya timu ya taifa.
Akitoa taarifa ya Kibu kupatiwa uraia wa Tanzania mwishoni mwa wiki, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene alisema nyota huyo aliyejiunga na Simba msimu huu akitokea Mbeya City amepewa uraia kufuatia ombi lililopelekwa kwake na TFF kupitia Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo.
Simbachawene alisema Kibu ambaye uraia wake wa asili ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), alipewa uraia wa Tanzania tangu Septemba 30 mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya Uraia, Sura ya 357 (Rejeo la 2002).
Waziri huyo alisema Kibu amekuwa akiishi nchini Tanzania tangu mwaka 1998, akiwa na umri wa miaka sita, baada ya wazazi wake kukimbia machafuko ya kisiasa DRC.
Akasema Kibu amekuwa na nyaraka zinazoonyesha yeye ni raia wa Tanzania, ikiwemo kitambulisho cha uraia, kwani yeye alikuwa anajijua ni Mtanzania kutokana na kuingia nchini akiwa na umri mdogo, na hana historia yoyote na nchi yake ya asili zaidi ya kukulia Tanzania.

0 comments:
Post a Comment