NDOTO za Simba Queens kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika zimezimwa leo baada ya kuchapwa 2-1 na wenyeji, Vihiga Queens katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati jioni ya leo Uwanja wa Moi Kasarani Jijini Nairobi nchini Kenya.
Mabao ya Vihiga Queens yamefungwa na Moren Achieng dakika ya 55 na Jentrix Chikangwa dakika ya 88 wakati la Simba Queens limefungwa na Aisha Juma Mnunka dakika ya 70.
Sasa Vihiga Queens itakutana na Commercial Bank FC iliyoitoa Lady Doves WFC ya Uganda kwa penalti 5-3 kufuatia sare ya 1-1 na fainali itachezwa Alhamisi.

Simba Queens itwania nafasi ya tatu dhidi ya Lady Doves, yakiwa marudio ya mchezo wa Kundi A ulioisha kwa sare ya 0-0.
Bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa dola za Kimarekani 100,000 pamoja na kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye mwaka huu nchini Misri – pia atapata dola 30,000 USD, mshindi wa pili dola 20,000 wa tatu dola 10,000.
0 comments:
Post a Comment