TIMU ya Namungo FC imeweka kambi wilayani Karatu mkoani Arusha kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Namungo FC inayofundishwa na kochw Mzanzibari, Hemee Suleiman 'Morocco' imeweka katika katika majengo ya akademi ya Black Rhino yenye Uwanja mzuri wa mazoezi na vifaa vingine vya kisasa.
Namungo FC yenye maskani yake Ruangwa mkoani Lindi imeboresha kikosi chake kwa kiasi kikubwa kwa kusajili wachezaji kadhaa wenye uzoefu wakiwemo waliowahi kucheza klabu za Azam, Simba na Yanga.
Hao ni pamoja na kipa David Kisu, washambuliaji Mzambia Obrey Chirwa kutoka Azam FC na Mkongo David Molinga 'Falcao' aliyewahi kucheza Yanga SC.
Wengine wapya ni Abdulmalik Zecharia, Abdulaziz Makame, Suleiman Bwenzi, Daniel Joram, Mohamed Issa 'Banka', Emmanuel Charles, Jacob Massawe, Vincent Philip, Baraka Mtuwi na Mwisho Yangson.
0 comments:
Post a Comment