BILIONEA mwenye asili ya Kiasia, Mohamed ‘Mo Dewji’ ametangaza kujiuzulu Uenyekiti wa Bodi ya Simba SC na kubaki mwekezaji pekee kwa umiliki wa asilimia 49 ya hisa zenye thamani ya Sh. Bilioni 20. Akitangaza uamuzi wake huo leo, Dewji amesema kwamba nafasi yake itashikiliwa na aliyekuwa Makamu wake, Salum Abdallah Muhene ‘Try Again’. "Muda umefika mimi kama Mohamed, tumefanya mkutano tarehe 21 mwezi wa tisa, 2021 na tumekubaliana kwamba mimi nitajiuzulu kuwa Mwenyekiti wa Simba Sports Club,".
"Naomba sana wana Simba msifikirie mimi nimeondoka kwenye Simba, bali bado ni mwekezaji kwenye Simba ni mwana hisa kwenye Simba, naipenda Simba na nitaendelea kuipenda Simba mpaka siku yangu ya mwisho," amesema Dewji leo Dares Salaam. Hatua hiyo inakuja siku moja tu baada ya timu kulazimishwa sare ya 0-0 na wenyeji, Biashara United katika mchezo wake wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jana Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara huku Nahodha, John Bocco akikosa penalti dakika ya 90. Januari 13 mwaka 2020 Mo pia alitangaza kujiuzulu Uenyekiti wa Bodi ya klabu hiyo na kubaki kama mwekezaji mara tu baada ya baada ya mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi uliomalizika kwa Simba SC kufungwa 1-0 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Kama ilivyokuwa mwaka jana, Mo Dewji alijiuzulu baada ya Simba SC kufungwa kwenye fainali ya Kombe la Kombe la Mapinduzi na safari hii anang'atuka timu ikitoka kutoa sare na Biashara na kufungwa na taini Yanva 1-0 katia Ngao yaJmii.
Lookman crowned African footballer of the year
-
The 2024 Confederation of African Football (CAF) Award took center stage on
Monday night, with the best talents in African football emerging winners.
The...
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment