MWILI wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe aliyefariki dunia Ijumaa jioni hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salam umeagwa leo katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali wa michezo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Leodegar Chilla Tenga wameshiriki zoezi hilo pamoja na wanachama wa Simba SC.
Mwili huo unatarajiwa kusafirishwa kesho kwa mazishi yatakayofanyika Jumatano Kihesa, Mkimbizi mkoani Iringa.
Hans Poppe alizaliwa Oktoba 15, mwaka 1956 mjini Dar es Salaam na kukulia mkoani Iringa na baada ya kumaliza elimu ya sekondari, alijiunga na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambako alifikia cheo cha Kapteni, kabla ya kuachishwa kazi na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela, kwa tuhuma za uhaini, dhidi ya serikali ya awamu ya kwanza, ya hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mwaka 1983.

Amekuwa mpenzi wa Simba SC tangu miaka ya 1970, akiwa kijana mdogo na zaidi mwenyewe aliwahi kusema, mechi ambayo ilimfanya ajitamke rasmi yeye ni Simba damu ilikuwa dhidi ya wapinzani wa jadi, Yanga Juni 23, mwaka 1973, ambayo Wekundu wa Msimbazi, walishinda 1-0, bao pekee la Haidari Abeid ‘Muchacho’ dakika ya 68.
Amekuwa Mjumbe Mteule wa Kamati ya Utendaji tangu mwaka 2010 na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili tangu 2012 kabla ya kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi katika mfumo mpya wa uendeshwaji klabu tangu mwaka jana. RIP Hans Poppe.
0 comments:
Post a Comment