MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Gulam Dewji amesema kwamba timu hiyo itakwenda Marekani mwakani kuweka kambi kwa mwaliko ya klabu ya D.C. United ya Washington D.C.
Mo Dewji amesema mwaliko huo ameupata baada ya kukutana na mmoja wa wamiliki wa D.C. United, Jason Levien anayemiliki kwa pamoja na Erick Thohir tangu mwaka 2012 walipoinunua.
"Ilikua ni furaha kukutana na Jason Levien, ambae ni mmiliki wa klabu ya mpira wa miguu ya DC United ambayo ina thamani ya dola za kimarekani millioni 700," amesema Mo Dewji na kuongeza;
"Nina furaha kutangaza ushirikiano mpya kati ya klabu za DC United na Simba. Ifikapo mwaka 2022, klabu ya Simba itasafiri kwenda Marekani kwa ajili ya mazoezi na maandalizi ya msimu mpya, na pia itashiriki katika mashindano ya kimataifa yatakayoandaliwa na klabu ya DC United, ambayo yatahusisha timu za ligi ya MLS na vilabu kutoka Amerika ya Kusini,".
0 comments:
Post a Comment