KATIKA kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, klabu ya Tanzania Prisons SC ya Mbeya imemsajili kipa Benedict Haule kutoka Azam FC na mshambuliaji Moses Kitandu kutoka Costa Do Sol ya Msumbiji.
Mkurugenzi wa Ufundi, Kelvin Fredinand amesema Kitandu ni Mtanzania aliyekuwa anacheza Ligi Kuu ya Msumbiji baada ya kuinukia timu ya vijana ya Simba SC na Haule aliyeibukia Mbao FC ya Mwanza alikuwa Azam FC kwa misimu miwili iliyopita.
0 comments:
Post a Comment