BONDIA mkongwe, Manny Pacquiao jana amepigwa kwa pointi na Mcuba, Yordenis Ugas katika pambano ambalo linaweza likawa la mwisho kwake lililofanyika ukumbi wa T-Mobile Arena, Jijini Las Vegas, Marekani kuwania ubingwa wa WBA uzito wa Super Welter.
Lakini Mfilipino huyo atakayetimiza miaka 43 baadaye mwaka huu hakutaka kusema atastaafu au la baada ya pambano hilo majaji wawili wakitoa pointi 116-112 kwa Ugas, na wa tatu 115-113.
Yordenis Ugas mwenye umri wa miaka 35 alipewa nafasi ya kupigana na Pacquiao wiki iliyopita tu baada ya mpinzani wa awali, Errol Spence Jr kujitoa kufuatia kuumia mazoezini.
0 comments:
Post a Comment