WENYEJI, Southampton wamelazimishwa sare ya 1-1 na Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa St. Mary's Jijini Southampton, Hampshire.
Kiungo Mbrazil, Frederico Santos 'Fred' alianza kujifunga dakika ya 30 kuipatia Southampton bao la kuongoza, kabla ya mshambuliaji wa kimataifa wa England, Mason Greenwood kuisawazishia Man United dakika ya 55 akimalizia pasi ya kiungo Mfaransa, Paul Pogba.
Man United inafikisha pointi nne katika mechi ya pili kufuatia ushindi wa 5-1 dhidi ya Leeds United kwenye mchezo wa ufunguzi, wakati Southampton inaokota pointi ya kwanza baada ya kuchapwa 3-1 na Everton wiki iliyopita.
0 comments:
Post a Comment