MWANAMUZIKI nguli barani Afrika, Koffi Olomide atatumbuisha kwenye tamasha la klabu ya Yanga lijulikanalo kama kilele cha Wiki ya Mwananchi Jumapili wiki hii Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Suma Mwaitenda amesema pamoja na gwiji huyo wa muziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), watakuwepo wasanii wengine mbalimbali wa nyumbani.
Tamasha hilo ni maalum kwa Yanga kuzindua rasmi msimu mpya kwa kutangaza kikosi chake pamoja na jezi itakazotumia nyumbani na ugenini msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment