// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HATIMAYE SIMBA SC YAMTAMBULISHA BEKI WAKE MPYA MKONGO, HENOC INONGA BAKA KUTOKA DC MOTEMA PEMBE YA KINSHASA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HATIMAYE SIMBA SC YAMTAMBULISHA BEKI WAKE MPYA MKONGO, HENOC INONGA BAKA KUTOKA DC MOTEMA PEMBE YA KINSHASA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, August 15, 2021

    HATIMAYE SIMBA SC YAMTAMBULISHA BEKI WAKE MPYA MKONGO, HENOC INONGA BAKA KUTOKA DC MOTEMA PEMBE YA KINSHASA


    KLABU ya Simba imemtambulisha beki Mkongo Henoc Inonga Baka kutoka DC Motema Pembe ya kwao, Kinshasa.
    Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye kwao anajulikana kwa jina la utani Varane, akifananishwa beki Mfaransa Raphael Varane mshindi wa Kombe la Dunia na mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya anakuwa mchezaji mpya wa tano Simba kuelekea msimu ujao.
    Wengine ni mawinga Msenegal, Papa Ousmane Sakho kutoka Teungueth Rufisque ya kwao, Yussuf Mhilu kutoka Kagera Sugar ya Bukoba na Mmalawi, Peter Banda kutoka Nyasa Big Bullet ya kwao, Blantyre.
    Simba SC ambayo tayari ipo kambini nchini Morocco kujiandaa na msimu mpya pia imemsajili kiungo Mmalawi, Duncan Nyoni kutoka Silver Strikers ya kwao, Lilongwe.
    Msimu ujao Simba itawakosa nyota wake wawili walioibeba timu kwa misimu miwili iliyopita, winga wa Msumbiji, Luis Miquissone aliyeuzwa Al Ahly ya Misri na kiungo Mzambia, Clatous Chama aliyeuzwa RSB Berkane ya Morocco.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HATIMAYE SIMBA SC YAMTAMBULISHA BEKI WAKE MPYA MKONGO, HENOC INONGA BAKA KUTOKA DC MOTEMA PEMBE YA KINSHASA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top