ARGENTINA imetinga fainali ya Copa America kwa ushindi wa penalti 3-2 kufuatia sare ya 1-1 na Colombia ndani ya dakika 120 Alfajiri ya leo Uwanja wa Brasília.
Shujaa wa Argentina alikuwa ni kipa wa Aston Villa, Emiliano Martinez, aliyeokoa penalti tatu za Colombia.
Mshambuliaji wa Inter Milan, Lautaro Martínez alianza kuifungia Argentina dakika ya saba akimalizia pasi ya Nahodha, Lionel Messi, kabla ya mshambuliaji wa Porto, Luis Díaz kuisawazishia Colombia dakika ya 61 akimalizia pasi ya Edwin Cardona.

Na kwenye mikwaju ya penalti, Messi, Leandro Paredes na Lautaro Martínez waliifungia Argentina huku Rodrigo De Paul pekee akikosa na kwa Colombia waliofunga ni Juan Cuadrado na Miguel Borja pekee walifunga huku Davinson Sánchez, Yerry Fernando Mina na Cardona wakikosa.
Sasa Argentina itakutana na wenyeji, Brazil katika fainali ya Copa America Jumapili Uwanja wa Jornalista Mário Filho, au Maracanã Jijini Rio de Janeiro, wakati Colombia itawania nafasi ya tatu dhidi ya Peru Jumamosi.
0 comments:
Post a Comment