SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema haliwezi kubadili Kanuni wala Katiba yake kuhusu uchaguzi wakati mchakato wa zoezi hilo unaendelea.
Hayo ni majibu kwa wadau mbalimbali waliolalamikia na kuiandikia TFF juu ya vipengele mbalimbali kuhusu uchaguzi ambavyo wanaona vina kasoro au mapungufu.
Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wadau mbalimbali wa michezo nchini, wakiwemo wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu uchaguzi wa TFF uliopangwa kufanyika Agosti 7 mwaka huu Jijini Tanga.
Wengi wanaamini vipengele vya kanuni na Katiba kuhusu uchaguzi vinalenga kuwasafishia njia viongozi waliopo madarakani wanaoomba tena ridhaa ya kuongoza shirikisho hilo, akiwemo Rais wa sasa, Wallace John Karia ambaye amekwishachukua fomu kugombea tena.
0 comments:
Post a Comment