![]() |
MBUNGE wa jimbo la Kinondoni (CCM), Tarimba Abbas amejitoa kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliopangwa kufanyika Agosti 7, mwaka huu Jijini Tanga.
Tarimba, Rais wa zamani wa klabu ya Yanga ni kati ya watu wanne ambao hawajarejesha fomu walizochukua kwa gharama ya Sh. 500,000, wengine ni mmiliki wa African Lyon, Rahim Kangenzi, Deogratius Mutungi na Zahor Mohammed.
Waliorejesha fomu kuwania Urais wa TFF pamoja na Rais wa sasa, Wallace Karia, wengine ni Nahodha wa zamani wa timu ya taifa na klabu ya Yanga, Ally Mayay Tembele, Evans Mgeusa, wanahabari Ally Saleh wa Zanzibar, Oscar Oscar wa Dar es Salaam na mwanamke pekee, Hawa Mniga ambaye ni mtumishi wa umma.
0 comments:
Post a Comment