WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhakikisha wanataja tarehe mpya ya mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga haraka iwezekanavyo.
Hatua hiyo inafuatia mchezo huo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara kutofanyika Jumamosi ya Mei 8 baada ya kutokea mkanganyiko wa muda wa kuanza hatimaye kuahirishwa.
Pamoja na hayo, Waziri Mkuu Majaliwa akizungumza Bungeni Jijini Dodoma leo pia ameagiza Wizara hiyo na TFF kushughulikia hatima ya mashabiki waliolipa viingilio kwa ajili ya mchezo huo.
"Tumeiagiza Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa kuhakikisha kwamba wanatoa taarifa haraka sana kwa Watanzania mchezo wenyewe utachezwa lini, lakini pia vile viingilio vya Watanzania waliokuwa wamenunua (tiketi) kuingia kwenye mchezo ule hatima yake ni nini,".
Waziri Mkuu amewasihi Watanzania hususan wapenzi wa michezo waliojiandaa kushuhudia pambano hilo la watani Jumamosi waipe muda Wizara ije kutoa taarifa ikishirikiana na TFF ili kujua hatima ya mechi hiyo kubwa.

0 comments:
Post a Comment