WAZIRI wa Habari Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa anatarajiwa kukutana na uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFaf) na klabu ya Yanga kumaliza tofauti zilizopo baina ya pande hizo mbili.
Hayo yamesemwa Katibu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, Dk Hassan Abbasi jana kufuatia tetesi za Yanga kutaka kufanya maandamano ya amani kupinga kile waanchoamini uonevu wa TFF dhidi yao.
"Nimesikia watu wanataka kuandamana sijui maeneo gani, hawa watu wa Yanga wanaona kwamba kuna matatizo kwenye TFF au kuna msimamizi fulani, sasa hizi kelele zimekuwepo muda mrefu, kwa hiyo huwezi Serikali ukasema watu wanataka kuandamana iwe ni kweli, wametishia au hawapo halafu Serikali ukasema umetulia tu, kwa hiyo nafikiri hilo limekwishachukuliwa hatua,".
"Kesho mheshimiwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo amewaita Yanga kuwasikiliza kuna nini, lakini pia amewaita TFF wenyewe kwa upande mwingine nao kuwasikiliza kwamba kuna nini hiki, Kisha taratibu zile za kawaida za kimfumo wa mpira na taratibu hizo zitafuatwa,".
"Lakini kesho hili ningeomba pia nilisistize kwamba kama kuna malalamiko yoyote, wadau watulie Serikali ipo, inasikiliza na vyombo vipo, yale yanayopaswa kubaki kwenye kanuni za michezo yatabaki, yanayohitaji mwongozo na maelekezo ya Serikali tutatoa, hivi ndivyo tunavyopaswa kwenda," amesema Dk. Abass mjini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment