Na Asha Kigundula, DAR ES SALAAM
MABINGWA wa Tanzania, Simba SC jana wameendeleza furaha kwa mashabiki wake baaada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya El Merreikh ya Sudan katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba jana yalifungwa na Luis Miquissone dakika ya 18, Mohamed Hussein 'Tshabalala' dakika ya 39 na Chris Mugalu dakika ya.
Na kwa ushindi huo Simba SC inafikisha pointi 10 baada ya kucheza mechi nne na kuendelea kuongoza kundi hilo kwa pointi tatu zaidi ya mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri.
Ushindi huo unamaanisha Simba SC inahitaji pointi moja tu katika mechi zake mbili za mwisho dhidi ya AS Vita hapa Dar es Salaam Aprili 2 na Al Ahly Jijini Cairo Aprili 9 ili kwenda Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Na hiyo ni baada ya jana, Al Ahly kuwachapa AS Vita 3-0, mabao ya Mohamed Sherif dakika ya sita, Mohamed Magdi Kafsha 19 na Taher Mohamed dakika ya 78 Uwanja wa Des Martyrs de la Pentecote Jijini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Manula, Shomari Kapombe, Muhammed Hussein, Kennedy Juma, Joash Onyango/ Erasto Nyoni dk43, Taddeo Lwanga, Bernard Morrison/ Jonas Mkude dk71, Muzamil Yassin/ Larry Bwalya dk46, Chris Mugalu/ Meddile Kagere dk71, Clatous Chama na Luis Miquissoine/ Francis Kahata dk83.
El Marreikh: Monged Elneel, Darren Mattocks, Al Gozoli Nooh/ Musab Kurdaman dk78, Wendy Panga, Ahmed Ahmed, Dhiya Mahjoub, Sifeldin Malik, Wagdi Awad/ Azam Osam dk78, Mohamed Alrashed/ Ahmed Yousif dk46, Hamza Zakaria na Ammar Kamaleldini/ Mohamed Abbas Gumaa dk86.
0 comments:
Post a Comment