Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MABINGWA watetezi, Simba SC leo wameponea chupuchupu kupoteza mechi nyumbani baada ya kulazimisha sare ya 1-1 na Tanzania Prisons leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Shukrani wake kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Jose Miquissne aliyeisawazishia bao hilo Simba SC dakika ya tano ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90.
Na hiyo ni baada ya Prisons, timu inayomilikiwa na Jeshi la Magereza nchini kutangulia kwa bao la Salum Kimenya dakika ya 55.
Prisons walipata bao hilo baada ya mshambuliaji Simba SC kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kope Mutshimba Mugalu kutoka kukosa penalti.
Na Tanzania Prisons ikatapa pigo lingine baada ya mchezaji wake tegemeo wa safu ya ulinzi, Jumanne Elfadhil Nimkiza kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 43.
Kwa sare hiyo, Simba inayofundishwa na Mfaransa Didier Gomes Da Rosa inafikisha pointi 46 baada ya kucheza mechi 20 na kuendelea kushika nafasi ya pili nyuma ya watani wao wa jadi, Yanga SC wenye pointi 50 za mechi 23.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Joash Onyango, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Perfect Chikwende/ Clautus Chama dk55, Muzamil Yassin/ John Bocco dk46, Chriss Mugalu, Rally Bwalya/Bernard Morrison dk66 na Luis Miquissone.
Tanzania Prisons; Jeremiah Kisubi, Salum Kimenya, Benjamkin Asukile, Vedastus Mwihambi, Nurdin Chona/Dotto Ramadhani dk34, Jumanne Elfadhil, Ezekia Mwashilindi, Lambert Sibiyanka, Samson Mbangula/ Kassim Mdoe dk72, Jeremiah Juma na Adili Buha.
0 comments:
Post a Comment