Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha wachezaji 25 cha Simba SC kimeondoka Dar es Salaam jioni ya leo kwenda Khartoum, Sudan kwa ajili ya mchezo wao wa tatu wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, El Merreikh Jumamosi.
Mechi hiyo itakayochezwa Saa 4:00 usiku Uwanja wa Al-Hilal Jijini Omdurman na kuonyeshwa moja kwa moja na chaneli ya ZBC2 inayopatikana kwenye kisimbusi cha Azam TV inafuatia Simba kushinda mechi zake mbili za awali nyumbani na ugenini.
Ilianza kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, AS Vita mjini Kinshasa kabla ya kwenda kuwachapa na mabingwa watetezi, Al Ahly 1-0 Dar es Salaam.

Kipa namba moja wa timu, Aishi Salum Manula aliyeumia juzi kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanznaia Bara, Simba SC ikiichapa JKT Tanzania 3-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam amepona na amesafiri pia.
Aishi aliumia baada ya kugongana na Danny Lyanga wa JKT Tanzania hadi kupoteza fahamu na kushindwa kuendelea na mchezo nafasi yake ikichukuliwa na Beno Kakolanya.Kikosi cha Simba kilichoondoka ni makipa; Aishi Manula, Beno Kakolanya, Ally Salim.
Mabeki; David kameta, Shomari Kapombe, Gardiel Michael, Peter Maduhwa, Mohammed Hussein, Joash Onyango, Pascal Wawa, Erasto Nyoni na Kennedy Juma.
Viungo; Thadeo Lwanga, Jonas Mkude, Rally Bwalya, Muzamil Yassin, Luis Miquissone, Hassan Dilunga, Ibrahim Ajibu, Miraj Athumani, Clatous Chama na Francis Kahata.
Washambuliaji; Meddie Kagere, John Bocco na Kope Mugalu.
0 comments:
Post a Comment