KIKOSI cha Simba SC kimerejea jana Jijini Dar es Salaam kutoka Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambako Ijumaa walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, AS Vita katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mabingwa hao wa Tanzania wanatarajiwa kuunganisha safari kwenda Musoma mkoani Mara kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Biashara United Alhamisi ijayo Uwanja wa Karume.

0 comments:
Post a Comment