MABINGWA watetezi, Juventus jana wameichapa AS Roma 2-0, mabao ya Cristiano Ronaldo na Roger Ibanez aliyejifunga katika mchezo wa Serie A Uwanja wa Allianz mjini Torino.
Ronaldo alifunga bao lake la 17 msimu huu akitoka kusherehekea kutimiza miaka 36 ya kuzaliwa na sasa Juve inafikisha pointi 42 baada ya kucheza mechi 20 na kusogea nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Serie A, ikizidiwa pointi tano na vinara, Inter Milan ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi mbele ya AC Milan yenye pointi 46 za mechi 20 pia PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment