• HABARI MPYA

        Monday, February 08, 2021

        BONDIA SPINKS ALIYEMPIGA MUHAMMAD ALI AFARIKI DUNIA

        BINGWA wa zamani wa ngumi za kulipwa duniani, Leon Spinks amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 67.
        Mmarekani huyo aliyempiga gwiji, Muhammad Ali, amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani kwa miaka mitano iliyopita. 
        Menejimenti ya Spinks, The Firm PR & Marketing imesema kwamba Spinks alifariki dunia Ijumaa jioni, mkewe Brenda Glur Spinks akiwa pembeni yake.


        Spinks (kushoto) katika picha iliyopigwa February 15, mwaka 1978 akimpiga ngumi ya puani Muhammad Ali mjini Las Vegas, Marekeni 

        PICHA ZAIDI GONGA HAPA



        Na baada ya kifo hicho, marafiki wachache tu wa karibu na wanafamilia wengine wameruhusiwa kuhudhuria msiba kwa sababu ya tahadhari dhidi ya virusi ya corona.
        Spinks, aliyejulikana kwa jina la utani, Neon Leon alicheza ngumi za kulipwa kuanzia mwaka 1977 hadi 1995 na alipata umaarufu baada ya kumshinda kwa pointi Ali katika pambano la raundi nane mwaka 1978. 
        Kabla ya kujiunga na ngumi za kulipwa, Spinks alilitumia Jeshi la wana Maji la Marekeni kwa miaka mitatu kuanzia 1973 hadi 1976 kabla ya kwenda kutwaa Medali ya Dhahabu ya Olimpiki mwaka 1976 mjini Montreal nchini nchini Canada 

        PICHA ZAIDI GONGA HAPA

        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: BONDIA SPINKS ALIYEMPIGA MUHAMMAD ALI AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry