AZAM FC jana imezinduka na kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC yalifungwa na kiungo mzawa Iddi Suleiman 'Nado' dakika ya tano akiiadhibu timu yake ya zamani na mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 30, wakati la Mbeya City lilifungwa na beki mzawa, David Mwasa dakika ya 69.

Kwa ushindi huo, Azam FC inayofundishwa na kocha Mzambia, George Lwandamina inafikisha pointi 36 baada ya kucheza mechi 20, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi sita na mabingwa watetezi, Simba walio nafasi ya pili.
0 comments:
Post a Comment