• HABARI MPYA

        Saturday, January 16, 2021

        YAHYA ZAYD AREJEA AZAM FC KWA MKOPO WA MIEZI SITA KUTOKA MISRI ALIPOKUWA ANACHEZA SOKA YA KULIPWA

        KLABU ya Azam FC imemrejesha kiungo wake mshambuliaji, Yahya Zayd, kwa mkopo wa miezi sita kutoka Pharco ya Misri.
        Zayd ni mmoja wa wachezaji walioibukia kwenye kituo cha Azam Academy kabla ya kumpandisha timu kubwa ya Azam FC na baadaye kuuzwa Ismailia ya Misri mwaka juzi ambayo nayo ilimuuza Pharco baada ya msimu moja.
        Kiungo huyo mshambuliaji anafunga usajili wa Azam FC dirisha dogo akiungana na kipa Mganda Mathias Kigonya na mshambuliaji Mkongo Mpiana Monzinzi.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: YAHYA ZAYD AREJEA AZAM FC KWA MKOPO WA MIEZI SITA KUTOKA MISRI ALIPOKUWA ANACHEZA SOKA YA KULIPWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry