KLABU ya Azam FC imemsajili kipa Mganda, Mathias Kigonya, kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Forest Rangers ya Zambia – hilo likiwa pendekezo ya Kocha Mkuu, Mzambia George Lwandamina.
Usajili wa Kigonya ni mapendekezo ya Kocha Mkuu wa Azam FC, George Lwandamina, ambaye anataka kuimarisha zaidi eneo hilo la langoni.
Kigonya ambaye yumo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda 'The Cranes', amekuwa na mchango mkubwa akiwa na Forest Rangers, baada ya kusimama vema akiwa katika milingoti mitatu langoni.
Kipa huyo hodari, ametwaa tuzo ya Kipa Bora wa msimu mara mbili mfululizo wa Ligi Kuu Zambia, msimu wa 2019 ((ligi ndogo) na 2019/2020.
Msimu uliopita, hakuruhusu wavu wake kuguswa (clean sheet) kwenye mechi 14 kati ya 23 alizoichezea Rangers na msimu huu amekusanya nne katika mechi 10 alizocheza hadi anatua Azam FC.

0 comments:
Post a Comment