Kwa mujibu wa Kova, haya ndiyo makosa matatu aliyokuwa akituhumiwa kuyafanya, pamoja na hukumu zake.
KOSA LA KWANZA: Kutohudhuria semina elekezi iliyohusisha wachezaji, benchi la ufundi na viongozi. Adhabu yake ni faini ya shilingi milioni moja (1,000,000).
KOSA LA PILI: Kuchelewa kuingia kambini wakati timu ilipokuwa ikijiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union. Adhabu aliyopewa ni karipio kali na faini ya shilingi milioni moja (1,000,000) pamoja na kuwekwa katika kipindi cha uangalizi cha miezi sita.
KOSA LA TATU: Kutoripoti kambini siku ya 26/12/2020 bila ruhusa. Katika tuhuma hizi, kamati haikumkuta na hatia baada ya kamati kutothibitisha pasipo shaka shitaka hilo.
MAAGIZO
Kamati imemtaka Mkude kurejea kambini mara moja kuendelea na mazoezi na asipofanya hivyo atakuwa amefanya tena kosa la utovu wa nidhamu.
Faini aliyotozwa anatakiwa kuilipa ndanI ya mwezi mmoja.
Kamati imemtaka Mkude kuomba radhi kwa maandishi ndani ya saa 24.
#HukumuYaMkude #JonasMkude #SimbaSC
0 comments:
Post a Comment