Na Anitha Jonas – WHUSM, DAR ES SALAAM
KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi amesema kuanzia mwaka 2021 kutakuwa Maonesho ya Kitaifa ya Sanaa za Ufundi nchini.
Dkt. Abbasi ametoa kauli hiyo leo Desemba 04, Jijini Dar es Salaam, katika mkutano na Wasanii wa Sanaa za Ufundi ikiwa ni mwendelezo wa vikao vyake vya kukutana na makundi mbalimbali ya wadau wa Sanaa kwa lengo la kujadili namna ya kukuza na kuendeleza sekta ya Sanaa kwa kuzingatia ahadi ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika hotuba yake wakati akifungua Bunge.
Akizungumza katika kikao hicho Dkt.Abbasi alisisitiza kuwa serikali imedhamiria kusaidia sekta ya sanaa, kwa kukuza masoko na kujenga mazingira rafiki ya kuendeleza sanaa nchini.

Akizungumza katika kikao hicho Dkt.Abbasi alisisitiza wasanii kutumia vyama vyao na Mashirikisho kutoa maoni ya mambo wanayokwamisha uendeshaji wa kazi zao ikiwemo utitiri wa kodi na tozo ambazo nikubwa zinazokwamisha shughuli hizo.
Naye Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa Taifa Godfrey Mngereza ahidi kupokea maoni yote ya wadau hao na kusema atayafanyia kazi ikiwemo kuandaa mpango wa kutoa mafunzo kwa wasanii wa Sanaa za Ufundi ya namna ya kufanya biashara katika mfumo wa kisasa kwa kuweka kipao mbele thamani ya kazi zao.
Halikadhalika nae Msanii wa Sanaa ya Uchoraji Hasmain Raza alitoa ombi kwa Serikali la kuangalia muundo wa majukumu kwa taasisi ya BASATA katika uendeshaji, kwa kuomba ianzishe Idara au Vitengo cha Muziki kwa kila sanaa wanayoisimamia, badala ya sasa hali ilivyo sasa vitu vyote kuendeshwa kwa pamoja.
0 comments:
Post a Comment